DHAMIRA

Ufumbuzi dhidi ya janga la mabadiliko ya tabia ya nchi umepatikana: Ni kuharakisha kufanya mabadiliko kwa kuacha nyuklia na mifumo ya hewa ya ukaa. Njia pekee ya uhakika ya kuzuia athari za mabadiliko ya tabia ya nchi yanayotokana na matumizi ya nishati ni kuhama haraka iwezekanavyo kutoka kwenye mfumo wa nishati ya zamani ya karne ya ishirini na vinu vyake vya nyuklia na tecnologia ya kutumia mafuta ya nyuklia (urani) ambavyo vinavyochafua hali ya hewa na tuelekee kwenye nishati mbadala ambayo ni Salama, safi, rahisi na ni technologia nzuri ya karne ya 21.

Nguvu za nyuklia kwa ujumla wake haziwezi kutatua tatizo la uchafuzi wa hali ya hewa. Kwa hakika ni kuendela kuharibu tabia ya nchi kwa kuzuia kuanzishwa kwa mifumo ya nishati safi.

Miongoni mwa matatizo mengi ya nishati za nyuklia ni:

Kutozingatia haki za binadamu na uharibifu wa mazingira. Watu wenye kipato cha chini na jamii yenye kipato cha chini wanalengwa kwa ajili uchimbaji wa migodi ya Urani na taka zenye mionzi mizito. Mionzi inaathiri wanawake na wasichana mara mbili zaidi ya kiwango inachoathiri wanaume. Na mionzo kwenye hewa kwa ujumla inaathiri vizazi vyote vijavyo na kuweka sumu mazingira kwa miaka mamia na maelfu.

  1. Mbaya Zaidi: Vinu vya nyuklia na mfumo wa uzalishaji wa nyuklia unazalisha kwa kiasi kikubwa mabaki yenye mionzi na sumu ambayo yanaongezeka kila unapotumia nishati ya nyuklia. Mfumo wa kutengeneza mafuta ya nyuklia (nuclear fuel chain) unazalisha hewa ya ukaa zaidi kuliko nishati mbadala ambayo haizalishi hewa ya ukaa. Kwa kawaida vinu vyote vya nyuklia vinazalisha mionzi na takataka za sumu. Wanasayansi wamekubaliana na kudhibitisha kuwa hakuna usalama kwenye mionzi.

  2. Hatari Zaidi: Kuendelea kutumia nguvu za nishati ya nyuklia kutasababisha matatizo zaidi ya yale ya Fukushima, Church Rocks na Chernobyl (Fukushima – Japani, Church Rocks – Marekani na Chernobyl-Ukraine: Maeneo ambayo yalipatwa na maafa ya nyuklia). Utaalam na malighafi zinazohitajika kutengeneza nishati ya nyuklia zinaweza zikabadilishwa na kuingiza kwenye mpango wa kutengeneza silaha ya kiini (nuclear weapons).

  3. Gharama zaidi: Nishati ya nyuklia inagharama zaidi katika kuondoa hewa ya ukaa na inahitaji uwekezaji mkubwa zaidi kuliko kuwekeza kwenye nishati mbadala.

  4. Polepole mno: Kutumia nishati ya nyuklia kwa lengo la kupunguza hewa ya ukaa itahitaji mpango wa ujenzi wa vinu vya uzalishaji wa nishati zaidi kwa makampuni kuliko uwezo wao na kwa muda uliopangwa.

Nishati mbadala na safi ni pamoja na umeme wa jua, upepo, geothermal, umeme uliohifadhiwa pamoja na nishati nyingine za kitaalam ambazo zinazokidhi mahitaji ya nishati bila kusababisha sumu, taka za mionzi na uchafuzi mwingine wa hewa.